Kombe la Dunia kwa mabanati kuanza kutifua vumbi leo Dominica

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya 17 ya fainaliza Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17,  yatang’oa nanga leo usiku katika Jamhuri ya Dominica.

Nigeria watafunfua dimba kundini A dhidi ya Newzealand, kabla ya Uhispania kumenyana na Marekani pia saa tano usiku katika kundi B.

Wenyeji Dominican watashuka uwanjani saa nane usiku dhidi ya Ecuador, nao Korea Kusini waijulie hali Colombia, katika kundi B kuanzia saa usiku wa manane.

Kenya inayoshiriki kwa mara ya kwanza itafungua harakati zake kundini C Ijumaa usiku dhidi ya Uingereza.

Baadaye Kenya watakabana koo na Korea Kusini Jumapili usiku, kabla ya kukamilisha mechi za makundi Oktoba 24 dhidi ya Mexico.

Kikosi cha Junior Starlets  chini ya kocha Mildred Cheche,kinajivunia kutopoteza mechi yoyote ya kujipima nguvu katika michuano minne waliyocheza,kabla ya fainali hizo .

Kenya,Zambia na Nigeria ndio waakilishi watatu wa Afrika kwenye fainali hizo za nane za Kombe la Dunia.

Website |  + posts
Share This Article