Kocha wa Senegal Aliou Cisse apigwa kumbo

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la kandanda nchini Senegal limemtimua kocha mkuu wa timu ya taifa Aliou Cisse, kutokana na msururu wa matokeo mabaya ya timu hiyo katika mechi za kufuzu kwa kombe la Afrika mwaka 2025 na la Dunia mwaka 2026.

Cisse amekuwa usukani tangu mwaka 2015 na anakumbukwa kwa kuingoza Senegal kunyakua kombe la bara Afrika mwaka 2022 walipoibwaga Misri penati 4-2 kufuatia sare.

Cisse aliye na umri wa maiak 48 alikuwa nahodha wa  Simba wa Teranga walipofuzu kwa komeb la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2002 nchini Korea Kusini na Japan.

Kwenye fainali hizo Senegal waliwalaza mabingwa watetezi Ufaransa katika mchuano wa ufunguzi na pia kucheza hadi kwota fainali walipotimuliwa na Uturuki kupitia sheria ya bao la dhahabu.

Shirikisho la Senegal SFF limemshukuru kocha huyo kwa mchango wake timuni huku likianza mchakato wa kumsaka kocha mpya.

Website |  + posts
Share This Article