Kwa mara ya kwanza, wakazi wa kaunti ya Machakos watapata fursa ya kupata huduma za kisheria katika ofisi ya mwanasheria mkuu nchini bila kuhitajika kusafiri hadi jijini Nairobi au kusubiri kwa muda mrefu katika afisi ya mwansheria mkuu wakitafuta huduma hizo.
Hii ni baada ya kufunguliwa kwa kliniki spesheli ya masuala ya sheria katika afisi ya mwanasheria mkuu nchini katika kaunti hiyo.
Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu, afisi yake inapania kufungua matawi ya kiliniki za kisheria nchini kutoa huduma za kisheria kwa urahisi kwa wananchi katika kaunti zote.
Kliniki ya kwanza ikifunguliwa leo Alhamisi katika kaunti ya Machakos, na ya pili itafunguliwa katika kaunti ya Nairobi katika mahakama ya Kibera kwa lengo la kupunguza mrundiko wa kesi katika afisi hiyo.
Katika hotuba iliyosomwa na mwakilishi wake kwenye hafla ya ufunguzi huo ni kwamba hatua hii inapania kugatua afisi hiyo na kusaidia utoaji wa huduma za kisheria kwa uma kuhusu utata wa umiliki wa ardhi, maswala ya watoto, usimamizi wa sheria za serikali , maswala ya katiba na sheria ili kupunguza msongamani katila afisi za mwanasheria mkuu wa serikali .
Kliniki hiyo itakuwa ya kipekee nchini kufunguliwa katika kiwango cha kaunti ikipania kusaidia wananchi kutataua masuala yao ya kisheria pasipo kugharimika sana.
Mwanasheria mkuu akitoa wito kwa asasi za kishetia nchini kushirikiana kutoa huduma kwa wananchi ili kufanikisha idara ya sheria nchini.