Rais William Ruto leo Jumatano ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kimataifa cha kibiashara cha China na Kenya katika uwanja wa maonyesho ya kilimo wa Jamhuri jijini Nairobi.
Kituo hicho kitakachogharimu kitita cha shilingi bilioni tano na ambacho ni cha ukubwa wa mita 68,000 mraba, kitahifadhi maonyesho ya bidhaa, hoteli ya kifahari na vifaa vingine vya kisasa.
Rais Ruto alisema uwekezaj huo ni ishara ya kiwango cha juu cha imani ya uchumi wa taifa, ambao uko imara, na mandhari ya kutabirika inayowahakikishia wawekezaji mapato.
Kulingana na kiongozi wa taifa, kituo hicho kitatoa nafasi 3,000 za kazi Kwa raia wa hapa nchini.
“Hatua hii inaashiria mwanzo wa mabadiliko ya kiuchumi kwa taasisi za maonyesho ya kilimo, pamoja na kuhakikisha vifaa vya serikali vinatumika kuimarisha ukuaji,” alisema Rais Ruto.