Kitui mbioni kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi

radiotaifa
1 Min Read

 Serikali ya kaunti ya Kitui inaendesha mikakati mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri wa Mazingira wa kaunti hiyo Richard Mwendandu, amesema kuwa wizara yake imefanikiwa kuongeza kiwango cha misitu kwa kupanda miti, pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu kama vile sola ili kupunguza gharama ya umeme kwa wakazi.

Aidha, amewahimiza wakulima kuendelea kutekeleza kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi ili kuongeza mavuno na kupunguza uhaba wa chakula.

Share This Article