Bingwa mtetezi wa dunia Faith Kipyegon,Nelly Chepchirchir na Edinah Jebitok wamefuzu kwa nusu fainali ya Jumapili ya mbio za mita 1500,katika siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha ya Dunia mjini Budapest Hungary.
Jebitok alifuzu kwa nusu fainali baada ya kumaliza wa nne katika mchujo wa kwanza ,naye Kipyegon akaongoza mchujo wa pili huku Chechirchir akiongoza mchujo wa tatu.
Hata hivyo matumaini ya Purity Chepkurui kufuzu kwa semi fainali yaliyogonga mwamba baada ya kumaliza katika nafasi ya saba kutoka mchujo wa tatu.