Kipyegon na marehemu Kiptum ndio wanaspoti bora 2023

Dismas Otuke
3 Min Read
Faith Kipyegon

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Faith Kipyegon na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya Marathon marehemu Kelvin Kiptum, ndio wanaspoti bora wa mwaka 2023 katika makala ya 20 ya tuzo ya SOYA.

Kipyegon alikuwa na msimu wa kufana akivunja rekodi tatu za dunia ndani ya mwezi mmoja kando na kunyakua dhahabu mbili za dunia .

Bingwa wa dunia wa mbio za nyika Beatrice Chebet alimaliza wa pili huku bingwa dunia wa mita 800 Mary Moraa akichikua nafasi ya tatu.

Marehemu Kiptum alivunja rekodi ya dunia katika mbio za Chicago na kutwaa ubingwa wa London Marathon alitangazwa mshindi upande wa wanaume.

Mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 10000 Daniel Simiu Ebenyo alimaliza wa pili huku Daniel Wanyonyi akimaliza wa tatu.

Washindi wa tuzo za SOYA mwaka 2023

Mwanaspoti bora Wanaume
1. Kelvin Kiptum (Athletics)
2. Daniel Simu (Athletics)
3. Emmanuel Wanyonyi (Athletics)
Mwanaspoti bora wanawake
1. Faith Kipyegon (Athletics)
2. Beatrice Chebet (Athletics)
3. Mary Moraa (Athletics)

Mwanaspoti bora walemavu wanaume
1. David Ngugi (Special Olympics-Cycling)
2. Kelvin Kipkogei (Deaf Athletics)
3. Titus Maundu (Para-Athletics)

Mwanaspoti bora walemavu wanawake
1. Asiya Sururu ( Para-Rowing)
2. Purity Kandie (Special Olympics, Athletics)
3. Nancy Chelagat (Para-Athletics)

Timu bora wanaume walemavu

National Handball

Timu bira wanawake walemavu

Beach Volleyball

Timu bora ya mwaka wanaume
1. Kabras Sugar ( Rugby)
2. Roll Ball National Team
3. National Under 18 Football Team

Timu bora ya mwaka wanawake
1. 3×3 National Basketball Team
2. National Volleyball Team
3. Roll Ball National Team

Kocha bora wa mwaka
Evelyn Kidogo (Basketball)

Chipukizi bora wanaume
1. Ismael Kipkurui (Athletics)
2. Aldrine Kibet (Football)
3. Nathaniel Muchoki (Chess)

Chipukizi bora wanawake
1. Valerie Nekesa (Football)
2 Bianca Ngecu (Golf)
3. Nancy Cherop (Athletics)

Kocha bora shule

Isaac Muresia (Namwela)

Timu bora shule wavulana
1. Koyonzo (Rugby)
2. Namwela (Namwela)
3. St Anthony, Kitale (Football)

Timu bora shule wasichana
1. Kwathanze (Volleyball)
2. Nyamira (Hockey)
3. Buteere Girls High School (Football)

Hall of Fame

Henry Rono (Athletics)

Hafla hiyo iliandaliwa Ijumaa usiku katika ukumbi wa KICC na kuongozwa na Waziri wa michezo Ababu Namwamba.

Share This Article