Faith Kipoyegon baada ya kuhifadhi taji ya dunia ya mbio za mita 1500 Jumanne usiku mjini budapest Hungary kwenye mashindano ya dunia,ameingia kwenye madaftari ya kumbukumbu kuwa mwanariadha wa kwanza wa kike kunyakua mataji matatu ya dunia ya shindano hilo.
Kipyegon ambaye pia ni bingwa mara mbili wa Olimpiki amekuwa na mwaka 2023 wa kufana akivunja rekodi tatu za dunia za mita 1500,mita 5,000 na maili moja ndani ya miezi miwili, kabla ya kuhifadhi taji ya mita 1500 aliyokuwa ameshinda mwaka jana mjini Oregon Marekani.
Kenya kwa sasa imetwaa medali tatu ,dhahabu 1,fedha 1 na shaba 1 ikishikilia nafasi ya nne.