Kipyegon atwaa dhahabu ya pili ya Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa dunia katika mita 1500 Faith Kipyegon ndiye bingwa mpya dunia katika mita 5000,baada ya kuibuka mshindi Jumamosi usiku.

Kipyegon aliye na umri wa miaka 29 alitimka katika umbali mita 400 za mwisho akikstahimi ukinzani kutoka kwa Sifan jassan na kuzikamilisha mwa dakika 14 sekunde 53 nukta 88,akifuatwa na Hassan aliyeshinda frdha kwa dakika 54 nukta 11 huku bingwa wa Jumuiya ya madola Beatrice Chebet akiridhia shaba mwa dakika 14 sekunde 54 nukta 33.

Bingwa huyo wa Olimpiki mara mbili ni Mkenya wa tatu wa Olimpiki ni Mkenya wa tatu kutwaa dhahabu ya dunia baada ya Vivian Cheruiyot na Hellen Obiri walishinda mataji mawili kila mmoja.

Awali Emmanuel Wanyonyi alishinda medali ya fedha ya mita 800 akitimka kwa dakika 1 sekunde 44 nukta 53 nyuma ya Marco Arop wa Canada aliyechukua dakika 1 sekunde 44 nukta 24 kuzikamisha.

Kenya ni ya 7 katika jedwali la medali kwa dhahabu 2 fedha 2 na shaba 2.

Share This Article