Kipyegon atuzwa shilingi milioni 2 na Safaricom

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya kutoa huduma za mawasiliano ya Safaricom imemtuza Bingwa wa Dunia na Olimpiki Faith Kipyegon shilingi milioni 2.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo kuvunja rekodi mbili za dunia siku chache zilizopita.

Kipyegon mwenye na umri wa miaka 29, aliweka rekodi mpya za dunia katika mbio za mita 1500 ya dakika 3 sekunde 49 nukta 11, na mbio za mita 5000 ya dakika 14 sekunde 5 nukta 20 katika mikondo ya Diamond League ya Golden Gala na Paris mtawalia.

“Kuweka rekodi mbili za dunia ndani ya wiki moja lilikuwa jambo la kushangaza kwangu. Ilinishtua na hadi sasa ningali na mshtuko. Sikutarajia hili, ila bado naamini kuwa nilikuwa nimejiandaa vyema kukimbia vyema na kuweka muda bora wa binafasi. Naishukuru Safaricom kwa kutambua juhudi zangu na kunituza; hii ni ishara nzuri kwa wanariadha wa Kenya,” alisema Kipyegon.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa alimpongeza Kipyegon kwa matokeo hayo bora na kuitangaza Kenya ulimwenguni.

“Katika Safaricom, tumejitolea kusaidia na kukuza vipaji nchini. Tunamshuruku na kujivunia Faith kwa matokeo aliyoafikia, kuvunja rekodi mbili za dunia katika kipindi cha wiki moja. Nina imani hili litawatia motisha zaidi wengine walio na vipaji nchini Kenya,” alisema Ndegwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *