Bingwa mara tatu wa Olimpiki katika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon, amehifadhi taji ya mbio za maili moja za mashindano ya Athlos NYC nchini Marekani mapema Jumamosi.
Kipyegon ambaye pia ni bingwa wa mara nne wa Dunia amezitimka mbio hizo kwa dakika 4 sekunde 17.78.
Nafasi ya pili ilimwendea Gudaf Tsegay kutoka Ethiopia kwa dakika 4 sekunde 19.75, huku Nikki Hiltz wa Marekani akiridhia nafasi ya tatu kwa muda wa dakika 4 sekunde 32.51.
Mkenya mwingine Susan Ejore alimaliza wa tano.