Kipyegon afuzu fainali huku Cheruiyot akikosa kufuzu katika mita 1500

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mtetezi wa dunia katika mita 1500 Faith Kipyegon amejikatia tiketi kwa fainali  baada ya kuongoza mchujo wa pili wa nusu fainali mjini Budapest Hungary Jumapili jioni.

Kipyegon aliongoza kwa dakika 3 sekunde 55 nukta 14 huku pia Nelly Chepchirchir akifuzu baada ya kuongoza nusu fainali ya kwanza kwa muda wa dakiak 4 sekunde 2 nukta 14, wakati Edinah Jebitok akikosa baada ya kuambulia nafasi ya kumi.

Fainali ya wanaume itakuwa na Abel Kipsang na Reynold Kipkorir huku bingwa wa dunia mwaka 2019 Timothy Cheruiyot akikosa kufuzu kwa fainali.

Fainali ya akina dada itaandaliwa Agosti 22 huku ile ya wanaume ikiandaliwa tarehe 23.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *