Makala ya 34 ya patashika ya kuwania kombe la AFCON itaanza rasmi Jumamosi usiku Januari 13 nchini Ivory Coast .
KBC Channel 1 itakuletea mubashara sherehe za ufunguzi na mechi ya kwanza ya kundi A kati ya wenyeji dhidi ya Guinea Bissau kuanzia saa tano usiku.
Kumbuka mechi zote 52 zitakujia mubashara kupitia runinga za KBC Channel 1 na Y254 na kutangazwa kupitia idhaa zote 13 za redio kwa lugha uipendayo.