Kelvin Kiptum ameweka rekodi mpya ya dunia katika marathon ya saa 2 na sekunde 35 katika mbio za Chicago Marathon nchini Marekani.
Kiptum ambaye pia ni bingwa wa London Marathon mwaka huu amevunja rekodi ya awali ya saa 2 dakika 1 na sekunde 9 iliyoandikishwa na bingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge mwaka 2022 katika mbio za Berlin Marathon.
Mshindi wa mwaka jana Benson Kipruto amemaliza wa pili kwa saa 2, dakika 4 na sekunde 2 huku Abdi Bashir wa Ubelgiji akimaliza wa tatu.
Sifan Hassan wa Uholanzi ameshinda mbio za wanawake akisajili muda wa saa 2, dakika 13 na sekunde 44, akifuatwa na bingwa mtetezi Ruth Chepng’etich wa Kenya kwa saa 2, dakika 15 na sekunde 37.