Kiptum ateuliwa kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum ameteuliwa miongoni mwa wanariadha 11, wanaowania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka huu kwa wanaume..

Kiptum ameshinda mbio za London na Chicago marathon mwaka huu kando na kuweka rekodi mpya ya dunia ya marathon ya saa 2  na sekunde 35.

Wegine wanaowania tuzo hiyo ni mabingwa wa dunia Neeraj Chopra wa India ,Ryan Crouser wa Marekani,Mondo Duplantis wa Uswidi,Soufiane El Bakkali, wa Morocco ,Jakob Ingebrigtsen,wa Norway, Pierce LePage kutoka Canada,Noah Lyles wa Mrekani, Alvaro Martinwa Uhispania ,Miltiadis Tentoglou na Karsten Warholm wa Norway.

&nbspMshindi atabainika kupitia kwa kura zitakazopigwa na mashabiki mitandaoni ambapo unahitaji kuweka “like” kwa mwanariadha unayempigia kura katika mitandao ya Facebook, X, Instagram na YouTube na upigaji kura utafungwa Oktoba 28, kabla ya Baraza Kuu la Shirikisho la Riadha Duniani kupiga kura ambayo itakuwa asilimia 50.

Waaniaji tuzoya mwanariadha bora wa mwaka

Orodha hiyo itapunguzwa hadi wanariadha watano kati ya Novemba 13 na 14 na mshindi kubainika Disemba 11.

Website |  + posts
Share This Article