Kiprop na Chepkorir washinda mbio za marathaon Iten

Dismas Otuke
1 Min Read

Luke Kiprop na Naomi Chepkorir ndio mabingwa wa mbio za marathoni za Iten zilizoandaliwa Jumapili mjini Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Kiprop aliye na umri wa miaka 20 ameshinda mbio za wanaume kwa muda wa saa 2 dakika 13 na sekunde 19, akifuatwa na Charles Kimeli kwa saa 2 dakika 14 na sekunde 26 huku Edwin Yator akiridhia nafasi ya tatu kwa saa 2 dakika 14 na sekunde 45.

Naomi Chepkorir ameshinda mbio za wanawake kwa kutumia saa 2 dakika 32 na sekunde 36, akifuatwa na Linah Kaino kwa saa 2 dakika 34 na sekunde 27 naye Caroline Kimosop akamaliza wa tatu kwa saa 2 dakika 36 na sekunde 36.

Share This Article