Kipchoge na Kipruto kuzua mhemuko Berlin Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mtetezi wa mbio za Berlin Marathon Eliud Kipchoge na bingwa wa London marathon mwaka 2022 Amos Kipruto watapambana katika makala ya 49 ya mbio hizo siku ya Jumapili.

Kipchoge ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki anawania taji ya tano ya Berlin Marathon, alikoweka rekodi mpy ya dunia ya saa 2 dakika 1 na sekunde 9 mwaka uliopita.

Amos Kipruto akishinda London marathon mwaka 2022

Wachanganuzi wamebashiri uwezekano wa rekodi ya dunia kuvunjwa ikizingatiwa kasi ya Kipruto na ya Kipchoge.

Ni mara ya pili kwa Kipruto na Kipchoge kushindana baada ya Kipchoge kushinda mbio za Tokyo Marathon mwaka uliopita huku Kipruto akimaliza wa pili.

Share This Article