Kipchoge and Chepkirui wako ange kwa New York City Marathon Jumapili

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge atashiriki mbio za New York City Marathon kwa mara ya kwanza Jumapili Novemba 2, huku Kenya ikiwakilishwa na kikosi madhubuti kwa wanaume na wanawake.

Kipchoge anayejivunia muda wa kasi wa saa 2 dakika 1 na sekunde 9, atashiriki makala hayo ya 54 pamoja na mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki Benson Kipruto, Alexander Mutiso , Abel Kipchumba na bingwa wa zamani Albert Korir .

Wakenya watapata ukinzani kutoka kwa bingwa mtetezi Abdi Nageeye wa Uholanzi na Waethiopia Kenenisa Bekele na Deresa Geleta, pamoja na bingwa wa Dunia, Alphonce Felix Simbu kutoka Tanzania.

Bingwa mtetezi Sheila Chepkirui atashiriki mbio za wanawake pamoja na bingwa Sharon Lokedi, mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki Hellen Obiri, mshindi wa nishani ya shaba mwaka jana Vivian Cheruiyot, na bingwa wa mwaka 2010 Edna Kiplagat.

Website |  + posts
Share This Article