Mikrofoni ya Cardy B yauzwa dola elfu 99.9

Marion Bosire
1 Min Read

Mikrofoni ambayo mwanamuziki wa Marekani Cardi B alimrushia shabiki aliyemkosea heshima kwa kumtupia kinywaji mwezi jana huko Las Vegas kimeuzwa kwa dola elfu 99,900 kwenye mnada ulioendeshwa kwenye soko la mtandaoni la eBay.

Scott Fisher, mmiliki wa kampuni ya Wave Inc ambayo hukodisha vifaa vya kupaza sauti, ndiye aliuza mikrofoni hiyo. Siku hiyo, Wave Inc ilikuwa imepeleka vifaa vyake kutumika kwenye eneo la burudani la Drai’s Beachclub huko Las Vegas ambako Cardi B alikuwa akitumbuiza.

Julai 29, 2023, kwenye tukio ambalo lilinaswa kwenye video, Cardi B ambaye alikuwa na ghadhabu alionekana akimlenga shabiki kwa mikrofoni hiyo baada ya shabiki huyo kumrushia kinywaji. Shabiki huyo alimshtaki Cardi kwa maafisa wa polisi lakini mwanamuziki huyo hakuchukuliwa hatua yoyote.

Fisher aliitafuta mikrofoni hiyo na kuamua kuiuza na anasema pesa ambazo amepata kutokana na mauzo hayo zitasaidia mashirika mawili ya usaidizi wa jamii ambayo ni “Friendship Circle Las Vegas” na “the Wounded Warrior Project”.

Fisher anasema watu wapatao 120 walionyesha nia ya kununua mikrofoni hiyo ambayo bei yake ya kawaida madukani ni dola elfu moja.

Awali, alitarajia kuiuza kwa dola elfu tano lakini akapata mnunuzi wa mwisho wa dola elfu 99, 900.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *