Kioni amshutumu Gachagua kwa kutumika kuwatenganisha watu wa Mlima Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee anayekabiliwa na utata Jeremiah Kioni amemshutumu Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kutumika na viongozi wengine kuwatenganisah wakazi wa eneo la Mlima Kenya.

Akizungumza mjini Nyahururu, Kioni amemkosoa Gachagua kwa matamshi yake kuwa Kenya ni nchi ya wenye hisa.

Amedai matamshi hayo yana athari mbaya kwa wakazi wa Mlima Kenya na yanalenga kuleta mgawanyiko kwani Kenya ni taifa lililo na makabila zaidi ya 42 na sio makabila mawili tu.

Kioni pia alisema ni kinaya kwa Naibu Rais kutaka kuridhiana na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ambaye amekuwa akimkejeli kwa kila njia.

Mbunge huyo wa zamani pia ametetea mazungumzo yanayoendelea ya maridhiano katika ukumbi wa Bomas kati ya serikali na upinzani akisema yanafaa ili kuwezesha nchi kusonga mbele.

Share This Article