Kiongozi wa Hamas Marwan Issa auawa

Tom Mathinji
1 Min Read

Kiongozi wa Hamas Marwan Issa alifariki katika shambulizi la anga la Israel, afisa wa Ikulu ya Marekani Jake Sullivan amesema.

Akiwa naibu kamanda wa kijeshi, Bw Issa atakuwa kiongozi mkuu wa Hamas kufariki tangu vita vilipoanza tarehe 7 Oktoba.Kundi la Wapalestina, linalodhibiti Gaza, halijazungumzia rasmi ripoti za kifo chake.

Siku ya Jumatatu, Rais wa Marekani Joe Biden alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuhusu mwelekeo wa vita hivyo.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa Bw Issa aliuawa katika shambulizi la anga lililolenga eneo la chini ya kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Gaza wiki moja iliyopita.

Naibu kamanda wa tawi la kijeshi la Hamas, Brigedi za Izzedine al-Qassam, alichukuliwa kuwa mmoja wa watu wanaosakwa sana na Israeli.

Umoja wa Ulaya, ambao ulimweka kiongozi wa Hamas kwenye orodha yake nyeusi ya magaidi, ulimhusisha moja kwa moja na shambulio la Oktoba 7 lililoongozwa na kundi hilo ambalo liliua takriban watu 1,200 na kuzua vita.

Share This Article