Kiongozi wa muungano wa Azimio Raila Odinga leo Ijumaa asubuhi aliwasili katika kaunti ya Homa Bay na kulakiwa na Gavana wa kaunti hiyo Gladys Wanga.
Magavana James Orengo wa Siaya na Ochilo Ayacko wa Migori ni miongoni mwa viongozi waliokuwapo kumlaki.
Wakati wa ziara yake Homa Bay, kiongozi huyo wa chama cha ODM anatarajiwa kufungua uwanja wa michezo wa Raila Odinga na Bustani ya Magavana ya Genowa.
Hata hivyo, anatarajiwa kutumia fursa hiyo kuendelea kuukosoa utawala wa Kenya Kwanza hasa kutokana na hatua ya kupitishwa bungeni na kutiwa saini kwa Mswada wa Fedha 2023 na Rais William Ruto.
Azimio inadai kutiwa saini kwa mswada huo kuwa sheria kutafanya maisha kuwa magumu zaidi na sasa inataka mswada huo utanguliwe.