Kindiki: Serikali imejitolea kuimarisha mapato yanayotokana na mifugo

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki ashiriki mkutano na wadau wadau wa sekta ya Mifugo.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki amesema serikali inajizatiti kuimarisha kibiashara sekta ya mifugo, kuongeza mapato kutoka kwa mifugo na bidhaa zake kama vile, maziwa, nyama na ngozi.

Akizungumza siku ya Jumanne, alipopokea taarifa kutoka idara ya ufugaji kuhusu hatua zilizopigwa kuboresha sekta hiyo, Naibu huyo wa Rais alidokeza kuwa baadhi ya hatua za serikali za kuhakikisha sekta ya ufugaji inanawiri ni pamoja na utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa kuwachanja mifugo, uboreshaji wa kiwanda cha ngozi nchini na kuhakikisha wakulima wanafaidika kutokana na mapato ya uuzaji maziwa

“Mapato kutokana na uuzaji wa maziwa umeongeeka pakubwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutoka shilingi bilioni 4.9 mwaka 2022 hadi shilingi bilioni 7.5 mwaka 2023 na kisha kuongezeka hadi shilingi bilioni 9.5 mwaka 2024,” alisema Prof. Kindiki

Katibu katika idara ya ustawishaji mifugo Jonathan Mueke, aliongoza ujumbe huo katika afisi ya Naibu Rais Mtaani Karen.

Hivi majuzi serikali ilianzisha mpango wa kitaifa wa kuwachanja mifugo, kwa lengo la kuangamiza magonjwa ambayo huwaathiri mifugo kama vile ule wa miguu na midomo.

Website |  + posts
Share This Article