Kindiki kuanzisha mashindano ya WRC Safari Rally Alhamisi

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki anatarajiwa kuanzisha mashindano ya mbio za magari ya mwaka huu ya WRC Safari Rally, yatakayoanza leo Alhamisi jioni mjini Naivasha.

Mashindano hayo yataanzishwa rasmi katika kituo cha mafunzo na utafiti wa wanyama pori (WRTI) mjini Naivasha.

Jumla ya magari 45 yatashiriki mashindano hayo ya kimataifa ya siku nne ambayo yatakamilika Jumapili.

WRC Safari Rally ni mashindano ya tatu mwaka huu kwenye kalenda ya mashindano ya mbio za magari baada ya yale ya Monaco mwezi Januari na yale ya mwezi jana nchini Uswidi.

Madereva watashindana kupitia vituo 20 vinavyojumuisha masafa ya kilomita 338.

Baadhi ya madereva mashuhuri watakaoshiriki mashindano hayo ni bingwa mara mbili Sebastien Ogier wa Ufaransa kutoka kampuni ya Toyota, mshindi wa mwaka jana Elfyn Evans pia wa Toyota, na Katsuta Takamoto kutoka Japani.

Kampuni zingine  za magari zinazowakilishwa ni Hyundai na Ford.

Madereva mashuhuri wa humu nchini ni pamoja na bingwa mara kadhaa wa kitaifa Carl Tundo, Pauline Sheghu na Leo Varese, miongoni mwa wengine.

Mashabiki watatazama magari hayo katika vituo kadhaa vilivyotengwa mbugani Naivasha na viunga vyake.

Share This Article