Kindiki azindua mashindano ya mbio za magari Naivasha

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki azindua mashindano ya mbio za magari WRC Safari Rally Kenya.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, leo Alhamisi amezindua rasmi mashindano ya mbio za magari ya WRC Safari Rally Kenya mjini Naivasha, huku akitaja mashindano ya mwaka huu kuwa magumu zaidi hasaa kutokana na msimu wa mvua unaoshuhudiwa hapa nchini.

Huku akidokeza kuwa serikali imewekeza kitita cha shilingi milioni 400 kwenye mashindano hayo, Kindiki alisema serikali imejitolea kuwekeza zaidi katika sekta ya michezo, akibainisha kuwa kwa sasa michezo imekuwa njia muhimu ya ajira kwa vijana wengi.

“Nashukuru mashirika ya umma na yale ya kibinafsi kwa kufadhili mashindano haya,” alisema Prof. Kindiki.

Kulingana na Kindiki shule maalum za udereva wa magari ya mashindano zenye vifaa kamili zimeanzishwa ili kusaidia kubaini na kufundisha vijana wenye vipaji katika mchezo wa rally.

Mashindano hayo yanayowashirikisha madereva 45, wakiwemo 17 wa Kenya yatakamilika siku ya Jumapili.

Share This Article