Kindiki awaonya waeneza chuki nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Usalama wa kitaifa Kithure Kindiki ameonya kuwa hakuna mtu aliye na uhuru wa kueneza chuki na migawanyiko miongoni mwa Wakenya.

Akizungumza katika kaunti ya Marsabit Jumatatu, Kindiki alisema hata ingawa Kenya inafurahia demokrasia imara na uhuru, hakuna mtu anayeruhusiwa kueneza mgawanyiko kwa misingi yoyote.

Alikuwa katika kaunti hiyo kwa uzinduzi wa sehemu ya nne na ya mwisho ya mMpango wa ruwaza ya Kenya 2030.

Kindiki alionya kuwa yeyote anayefikiri kuwa anaweza kutumia njia hizo kugawanya nchi ili kufikia malengo yake hana nafasi nchini.

Waziri alisisitiza kuwa serikali iko tayari kuwachukulia hatua wale wanaojaribu kuwachochea watu, bila kujali miegemeo yao ya kisiasa.

Alibainisha kuwa baadhi ya watu hao wanajificha nyuma ya vyama vya siasa kwa sababu ni washirika wa serikali iliopo akisema hawatasazwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *