Kindiki atetea polisi dhidi ya madai ya upendeleo

Marion Bosire
1 Min Read
Waziri wa Usalama Prof. Kithure Kindiki.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki ametetea maafisa wa usalama dhidi ya madai ya upinzani kwamba wanapendelea upande mmoja kisiasa.

Kindiki anasema maafisa wa polisi hawajihusishi na siasa kwa vyovyote bali wanaangazia jukumu lao kuu la kulinda mali na maisha ya Wakenya, kulingana na sheria zao za kazi.

Akizungumza katika hafla ya ibada, Waziri Kindiki aliwaomba wanasiasa wajiepushe na vurugu na badala yake wawe wakitumia mazungumzo. Alionya kwamba hakuna yeyote atakubaliwa kutishia na kusaliti Wakenya.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amemkosoa Inspekta Mkuu wa Polisi Japhet Koome kuhusu jinsi alivyokabiliana na maandamano humu nchini.

Hata hivyo, Kindiki amesema kwamba vurugu haifai kuwa suluhisho mbadala iwapo mazungumzo yanayoendelea kati ya serikali na upinzani yatashindikana.

“Wanasiasa wameanzisha mazungumzo. Wanapojadili masuala mbalimbali, lazima tuwakumbushe kwamba vurugu haifai kuwa sehemu ya suluhisho. Wasipokubaliana, hakuna atakayeruhusiwa kutishia na kusaliti watu wa Kenya,” alisema Waziri Kindiki.

Mazungumzo ya pande mbili kati ya mrengo wa Kenya Kwanza na ule wa Azimio la Umoja One Kenya yanaanza rasmi leo Jumatatu, Agosti 14, 2023.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *