Kindiki: Asilimia 93 ya nishati ya Kenya ni kawi safi

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki.

Kenya imepiga hatua kubwa kuhakikisha upatikanji wa kawi safi hatua ilinayofanikisha upishi salama bila kuharibu mazingira.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki amesema kuwa asilimia 93 ya nishati ya Kenya, ni nishat mbadala, akishiria kuwa hii ndio asilimia ya juu zaidi duniani.

Aidhi, kindiki alidokeza kuwa kenya pia imeafikia hatua muhimu katika kutumia madini muhimu yanayohitajika hasa magari ya umeme, betri, na teknolojia ya nishati mbadala.

Akizungumza Ijumaa katika Kongamano la Kitaifa kuhusu Uwekezaji lililoangazia jinsi ya kutumia nishati isiyoharibu mazingira(AGII), naibu huyo wa rais, alikiri kuwepo mapungufu katika kupata uwekezaji wa kutosha kufanikisha uzalishaji wa mbadala wa nishati isiyoharibu mazingira, uongezaji wa thamani kwa madini muhimu, kupika kwa kutumia kuni katika mamilioni ya familia, shule, hospitali, vituo vya kurekebisha tabia, na viwanda vya Majani Chai kwa njia safi, nafuu na endelevu kwa mazingira

“Serikali inajizatiti  kuimarisha uwazi wa sera, uhakika wa udhibiti, na ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ili kuziba mapengo haya na kuiweka Kenya kwa kizazi kijacho kwa ukuaji wa uchumi duniani,” alisema Kindiki.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Maafisa Wakuu serikalini, Wanadiplomasia na viongozi wa sekta ya kibinafsi kutoka mataifa 66 ya ughaibuni.

Share This Article