Kampuni ya Kinangop Dairy Limited ilitawala makala ya tano ya tuzo za kila mwaka za Kenya Beverage Excellence Awards (KBEA),zilizoandaliwa jijini Nairobi jana .
Kinangop Dairy ilimaliza ya pili katika vitengo vya Most preferred Long Life Milk na Most Preferred Kid’s Yoghurt Category .
Pia Kinangop Dairy ilichukua nafasi ya tatu katika kitengo cha Most Preferred Mala/Lala Milk .
Katibu katika Wizara ya viwanda Dkt.Juma Mukhwana aliyekuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo, aliihongera kampuni hiyo kwa mchango wake wa kubuni nafasi za ajira nchini.
Dkt. Mukhwana,pia alisifia mchango mkubwa wa sekta ya usindikaji maziwa nchini katika ukuaji wa uchumi na pato la kitaifa na kuongeza tija.
Tuzo za Kenya Beverage Excellence husherehekea uvumbuzi na ufanisi katika sekta ya usindikaji vinywaji.
“Tuzo hizi zinaashiria hatua kubwa zilizopigwa na kampuni ya maziwa ya Kinangop na pia ushahidi tosha kuhusu kujitolea kwetu kutengeza bidhaa bora na za kuaminika kwa wateja wetu”akasema meneja msaidizi wa bidhaa wa Kinangop Dairy Shivla Mathenge