Tukio la Kitropiki la kimbunga cha Hidaya lililotarajiwa katika pwani za Kenya na Daresalaam nchini Tanzania limekamilika rasmi baada ya upepo huo kufifia.
Serikali za Kenya na Tanzania zimetangaza kukamilika kwa tukio hilo rasmi siku ya Jumapili.
Kulingana na taarifa kutoka kwa idara za utabiri wa hali ya anga nchini Tanzania upepo huo uliokadiriwa kuwa wa kasi ya mafundo 40, ulikuwa hafifu ulipotua Jumamosi na kusambaratika kisha ukatoweka bila madahara yoyote .
Pia hali ilikuwa hiyo katika pwani ya Kenya baada ya idara ya hali ya anga kusema upepo huo ulififia na kutoweka .
Hata hivyo serikali za mataifa ya Tanzania na Kenya zimewatahadhari wananchi kuendelea kuwa macho na kutekeleza shughuli za baharini kwa uangalifu mkubwa.