Kim Kardashian na Lewis Hamilton waweka wazi penzi lao

Wameonekana pamoja jijini Tokyo nchini Japan ambapo walikwenda kwa likizo.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamitindo wa Marekani Kim Kardashian dereva mahiri wa Formula 1 Lewis Hamilton hawafichi tena uhusiano wa karibu kati yao.

Hii ni baada ya wawili hao kusafiri pamoja hadi nchini Japan kwa ajili ya likizo. Mpita njia mmoja alitambua wawili hao jijini Tokyo akawapiga picha na kuchapisha mitandaoni.

Kim na Lewis wanaonekana kutabasamu kwa furaha kwenye picha hizo.

Wawili hao ambao ni maarufu nchini Marekani wamekuwa wakionekana pamoja katika hafla mbali mbali na hivyo kuchochea uvumi kwamba wako kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Walionekana kwenye ndege ya kibinafsi barani Ulaya, ambapo walihudhuria sherehe ya mwaka mpya huko Aspen na katika awamu ya 60 ya Super Bowl huko California.

Vyanzo vinaelezea uhusiano huo kama wa kawaida na wa kufurahisha, huku wawili hao wakiona mambo yataendaje.

Wamekuwa marafiki kwa zaidi ya muongo mmoja, wakiwa wameonekana pamoja hadharani miaka ya 2014, 2021, na 2023.

Ingawa hakuna hata mmoja wao aliyethibitisha hadharani uhusiano huo, wameelezewa kuwa wanazidi kuwa karibu kimapenzi.

Share This Article