Familia ya Kardashian ina makala mengine mapya ya kipindi chao “The Kardashians” ambayo yanaonyesha Kim Kardashian ambaye alikuwa mke wa mwanamuziki Kanye West akidondosha machozi huku akisema amemkosa sana aliyekuwa mume wake na baba ya watoto wake.
Kwenye video fupi ya kutangaza makala yajayo, Kim anaonekana akizungumza na dadake Khloe akisema anatamani kurudiana na mume wake lakini hamtaki alivyo kwa sasa. Angependa arejelee hali yake ya awali, kwani Kanye wa zamani ndiye alimfahamu na kumpenda sio wa sasa.
Khloe alikuwa amemuuliza Kim ikiwa alikuwa sawa Kim akaanza kulia na kuelezea kilichokuwa kikimkosesha raha.
Kim na Kanye walitengana rasmi mwezi Machi 2022 baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka 6. Wana watoto wanne ambao ni North wa miaka 10, Saint wa umri wa miaka 7, Chicago miaka 5 na Psalm wa miaka 4. Kim alisema inavunja moyo kuona mtu ambaye alimfahamu vizuri awali kugeuka kuwa tofauti kabisa.
Kanye West amekuwa akizungumziwa na wengi mitandaoni hasa baada ya kubadili mtindo wa maisha. Mwimbaji huyo alibadili jina na kujiita Ye na huwa anavalia mavazi ya kiajabu kila mara anapoonekana hadharani.