Kikosi Harambee Stars kwa mechi ya Gambia chatajwa

Dismas Otuke
2 Min Read

Kocha wa Harambee Stars Benni McCarthy, ametangaza kikosi kwa michuano miwili ya kundi F kwa kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao dhidi ya Gambia na Gabon.

Beki wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Manzur Okwaro ameitwa kikosini kwa mara ya kwanza, huku Ismael Gonzalez akirejeshwa baada ya kutemwa.

Wanadinga wanaopiga soka ya kulipwa Eric Johana Omondi, Daniel Francis Anyembe, na Richard Odada watajiungana na wenzao mjini Abidjan, Ivory Coast.

Kikosi kilichotajwa cha wanandinga 23 kinajumuisha:-

Makipa;Ian Otieno,Brian Bwire,Faruk Shikhalo

Mabeki;Jonestone Omurwa,Brian Mandela,Daniel Anyembe,Amos Nondi,Erick Ouma,Manzur Okwaro,Ronny Onyango

Kiungo;Anthony Akumu,Richard Odada,Ismael Gonzalez,Timothy Ouma,Eric Johana,Duke Abuya,Mohammed Bajaber,Ben Stanley Omondi

Washambulizi;Masud Juma,Jonah Ayunga,Elvis Rupia,John Avire,Michael Olunga

Kenya itamenyana na Gambia Alhamisi hii katika uwanja wa Allasane Ouattara nchini Ivory Coast, kwa mechi ya raundi ya tano, kabla ya kuwaalika Gabon Jumapili hii katika uga wa kitaifa wa Nyayo kwa mchuano wa sita.

Harambee Stars inakalia nafasi ya nne katika kundi hilo kwa pointi tano baada ya kucheza mechi nne, kwenda sare mbili, kupoteza moja na kushinda mechi moja.

Ivory Coast inangoza kwa alama 10 ikifuatwa na Gabon kwa pointi 9, huku Burundi ikishikilia nafasi ya tatu kwa alama 7.

Kikosi kilichotajwa kitaabiri ndege kesho kuelekea Abidjan kwa mchuano huo wa Alhamisi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *