Ujumbe wa kwanza wa wanariadha wa Kenya watakaoshiriki mashindano ya Dunia jijini Tokyo, Japani kwa makala ya 20 yatakayoandaliwa kati ya tarehe 13 na 20 mwezi huu.
Kikosi kilichoondoka kiliwajumuisha mshindi wa nishani ya shaba katika mita 3000 kuruka viunzi na maji Faith Cherotich, Nelly Chepchirir (800m), Reynold Cheruiyot (1500m), na Phanuel Kosgei (1500m) miongoni mwa wengine.
Kikosi hicho kiliongozwa na Naibu wa kwanza wa kamati ya Olimpiki Kenya, Barnaba Korir .
Faith Kipyegon na Mary Moraa ndio wanariadha pekee watakaotetea mataji ya mwaka 2023 mjini Budapest, Hungary.
Zaidi ya wanariadha 2,000 kutoka mataifa 200 wanashiriki mashindano ya mwaka huu wakiwemo mabingwa 38 kati ya 41 walionyakua dhahabu miaka miwili iliyopita.
Kikosi cha Kenya kinawajumuisha wanariadha 58.