Kikosi cha Kenya kwa Mashindano ya Dunia ya Mbio za Barabarani chabadilishwa

Dismas Otuke
2 Min Read

Mshindi wa nishani ya fedha ya dunia mwaka 2022 Stanley Waithaka amejumuishwa katika kikosi cha Kenya kitakachoshiriki mashindano ya dunia ya mbio za barabarani mjini Riga nchini Latvia baina ya Septemba 30 na Oktoba mosi mwaka huu.

Waithaka aliye na umri wa 23 amejumuishwa kikosini kutwaa nafasi ya mshindi wa nishani ya shaba ya dunia katika mita 5,000 mwaka huu Jacob Krop anayeuguza jeraha.

Chipukizi huyo awali alikosa kuhudhuria majaribio ya kitaifa ya kuteua timu ya kushiriki mashindano ya dunia ya Budapest,Hungary kutokana na jeraha la kinea.

Waithaka atashiriki mbio za kilomita 5 sawia na Nicholas Kimeli na Cornelius Kemboi.

Bingwa wa kitaifa wa mbio za mita 1,500 Kyumbe Munguti,amechukua nafasi ya bingwa wa amani wa dunia Timothy Cheruiyot katika mbio za umbali wa maili moja.

Munguti atashirikiana na Abel Kipsang na chipukizi Reynold Cheruiyot huku bingwa wa Hamburg Marathon Samuel Nyamai akiitwa kikosini kuchukuwa nafasi ya
Alexander Mutiso na atashirikiana na mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 10,000 Daniel Simiu na Benard Kibet.

Kikosi cha wanawake kitaongozwa na bingwa mara tatu wa dunia Faith Kipyegon atakayeshindana katika umbali wa maili moja akishirikiana na Nelly Chepchichir na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech.

Share This Article