Kesi ya ardhi inayozozaniwa yaendelea Nakuru

radiotaifa
1 Min Read

Taarifa ya Simon Ben

Kesi ya shamba la Ngongongeri lenye ukubwa wa ekari 2,600 lililopo eneo la Njoro, kaunti ya Nakuru iliendelea katika mahakama ya ardhi Nakuru.

Shamba hilo linazozaniwa na Shirika la Mosiemo na Chuo Kikuu cha Egerton.

Saroveya wa ardhi alitoa ushahidi wake katika mahakama hiyo, huku akijipata matatani kwa kutobeba stakabadhi muhimu alizofaa kuandamana nazo.

Aidha, aliyekuwa naibu kamishna wa ardhi pia alisimama kizimbani na kutoa ushahidi wake.

Kesi hiyo itaendelea Juni 17 na 18 mwaka huu, mashahidi zaidi wakitoa ushahidi.

 

Share This Article