Kesi dhidi ya Dishi na Kaunti yatupiliwa mbali

Tom Mathinji
1 Min Read
Kesi dhidi ya Dishi na Kaunti yatupiliwa mbali.

Jaji wa mahakama kuu ya Milimani Chacha Mwita ametupilia mbali kesi iliyopinga mpango wa lishe shuleni ‘almaarufu Dishi na Kaunti’, unaotekelezwa na serikali ya kaunti ya Nairobi.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Janet Ouko, aliyehoji kuwa umma haukushirikishwa katika mpango huo, huku akitaka fedha zinazotumiwa katika mpango huo, zitumiwe kujenga madarasa.

Jaji Mwita alisisitiza umuhimu wa mpango huo kwa wanafunzi akisema ni sharti maslahi ya wanafunzi yapewe kipaumbele.

Waziri wa afya katika kaunti ya ya Nairobi Suzanne Silantoi alisifia uamuzi huo, akisema utawafaidi watoto wengi katika kaunti ya Nairobi, hasa wale kutoka familia zisizojimuda.

Alidokeza kuwa mwanafunzi mmoja kati ya wanne awali alikosa kwenda shuleni kwa sababu ya njaa.

“Gavana Johnson Sakaja, alipea chakula kipaumbele shuleni, baada ya kugundua kuwa njaa ilisababisha wanafunzi wenzi kusoma masomo,” alisema Silantoi.

Silantoi pia alisema juhudi zinafanywa kupanua mpango huo,ili kunufaisha zaidi ya watoto 307,000

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *