Kenya yawarejesha kwao raia wanne wa Uturuki

Tom Mathinji
1 Min Read

Katibu katika wizara ya Mambo ya Nje Korir Sing’Oei, amesema kuwa raia wanne wa Uturuki waliokuwa wakiishi hapa nchini kama wakinbizi, wamerejeshwa kwao.

Kupitia ujumbe katika mtandao wa X, Katibu huyo alisema hatua ya kuwarejesha raia hao nyumbani, ilitokana na ombi lililowasilishwa na Uturuki.

“Kenya imethibitisha kuwa raia wanne wa Uturuki walirudishwa nchini mwao siku ya Ijumaa, tarehe 18 mwezi Oktoba mwaka 2024, kwa ombi la Serikali ya Uturuki,” ilisema taarifa hiyo ya Sing’Oei.

Kulingana na taarifa hiyo, serikali ya Kenya ulitoa wito kwa maafisa wa Uturuki kuwashughulikia wanne hao kwa taadhima kuu, kuambatana na Sheria za taifa na zile za kimataifa.

Katibu huyo alidokeza kuwa Kenya italinda na kupigia debe Sheria za wakimbizi kuambatana na Sheria zilizopo za Kitaifa na kimataifa.

Share This Article