Kenya yawapokea swara 17 aina ya Mountain Bongo kutoka Marekani

Kulingana na wataalam wa maswala ya wanyama pori, asili ya swara aina ya mountain bongo ni nchini Kenya, na iwapo watapatikana kwingineko, basi huashiria walichukuliwa hapa nchini.

Tom Mathinji
2 Min Read
Kenya yawapokea swara 17 aina ya Bongo.

Kenya imewapokea swara 17 aina ya mountain bongo kutoka Florida, Marekani hii ikiwa hatua muhimu katika juhudi za kuwahifadhi wanyama hao.

Likiwapokea wanyama hao katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA, Shirika la Huduma kwa Wanyamapori hapa nchini KWS, lilisema juhudi hizo zinalenga kuimarisha ulinzi wa wanyama hao walio katika hatari ya kuangamia kwa kuongeza idadi yao, kubuni nafasi za ajira na kuboresha maisha ya jamii.

“Tunapoongeza idadi ya swara aina ya mountain bongo, tunatarajia kuwapokea watalii wengi na hivyo kuongeza mapato kwa taifa hili. Pamoja tunaimarisha mustakabal endelevu kwa wanyamapori na jamii kwa jumla,” ilisema KWS kupitia ukurasa wa X.

Kulingana na wataalam wa maswala ya wanyama pori, asili ya swara aina ya mountain bongo ni nchini Kenya, na iwapo watapatikana kwingineko, basi huashiria walichukuliwa hapa nchini.

Kenya yawapokea swara 17 aina ya mountain bongo kutoka Marekani.

Akizungumza wakati wa kuwasili wa swara hao katika uwanja wa JKIA, waziri wa Utalii na Wanyamapori hapa nchini Rebecca Miano, alisema swara hao watahifadhiwa kwa muda katika kaunti ya Meru, kabla ya kuachiliwa baadaye.

Kulingana na waziri Miano, idadi ya swara hao inatarajiwa kuongezeka hadi 700 kufikia mwaka 2050.

Hatua ya kuwarejesha swara hao iliafikiwa baada ya mataifa yanayohifadhi swara hao, kufanya mazungumzo ya makubaliano na kusaini utaratibu wa kuwarejesha nchini mwao.

Website |  + posts
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *