Serikali ya Kenya inaunga mkono mazungumzo ya amani nchini Sudan yanayoendelea jijini Nairobi.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi amesema Kenya inahimiza na kuunga mkono majadiliano kwani ndio suluhu pekee ya kutatua mzozo wa Sudan.
Mazungumzo hayo yanashirikisha vyama vya kisiasa, makundi ya kijamii na makundi ya kijeshi.
Pande zote zimesaini makubaliano kuhusu mchakato wa kurejesha amani na kubuni serikali ya umoja wa kitaifa nchini Sudan.
Aidha, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje amekiri kuwa mchakato wa kuleta amani nchini Sudan una changamoto tele.
Ametoa wito kwa pande husika kwenye mzozo huo kuwa na uaminifu.