Kenya imesaini mwafaka wa makubaliano na chama cha mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, utakaowezesha ukuzaji wa miundo msingi ta basketiboli nchini Kenya.
Mwafaka huo pia utawezesha ufunguzi wa afisi ya kikanda ya NBA jijini Nairobi
Mkataba huo umesainiwa mapema Ijumaa jijini Newyork kati ya Rais William Ruto na afisa mkuu mtendaji wa NBA Africa Victor Williams.
Waziri wa michezo Ababu Namwamba ameshuhudia kusainiwa na kuzinduliwa kwa mkataba huo.
Mwafaka huo utatoa fursa kwa wachezaji basketiboli nchini kukuza vipaji na kuimarisha maisha yao.