Kenya yamaliza ya pili Duniani katika Riadha

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imemaliza ya pili kwenye msimamo wa medali huku makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani yakikamilika Jumapili mjini Tokyo,Japan.

Kenya iliyokuwa ikiwakilishwa na wanariadha 58 imezoa jumla ya medali 11,dhahabu 7 fedha 2 na shaba 2.

Beatrice Chebet alinyakua dhahabu mbili (5000 na 10,000),Faith Kipyegon(1500m) Emmanuel Wanyonyi (800m)Faith Cherotich(3000msc) na Peres Jepchirchir (Marathon).

Washindi wa nishani za fedha walikuwa Faith Kipyegon mita 5000 na Dorcas Ewoi mita 3000 kuruka viunzi na maji  huku Edmund Serema akinyakua shaba ya mita 3000 kuruka viunzi na maji na Raynold Cheruiyot mita 1500.

Aidha Wakenya walivunja rekodi tatu za mashindano hayo wakiwa Wanyonyi,Cherotich na Odira.

Marekani ilitwaa ubingwa kwa medali 16 za dhahabu fedha 5 na shaba 5.

 

 

 

Website |  + posts
Share This Article