Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande maarufu Shujaa imehifadhi nafasi ya tisa, baada ya kuibwaga Samoa alama 10-5, katika mchuano wa mwisho wa Olimpiki Jumamosi jioni.
John Okeyo aliifungia Kenya Try moja kila kipindi na kuhakisha wamelipiza kisasi kushindwa na Fiji pointi 26-0, katika mechi ya kundi B wiki hii,ao Fiji wakazoa try ya pekee kupitia kwa Motu Opetai.
Mataokeo hayo yana maana kuwa Shujaa chini ya ukufunzi wa Kevin Wambua imehifadhi nafasi ya tisa waliyonyakua mwaka 2021.