Serikali ya Kenya imekubali pendekezo la serikali ya Qatar kuwekeza nchini katika miradi ya mafuta ,gesi,na mbolea huku nchi zote zikilenga kutanua mawanda ya ushirikiano na kuhuisha utangamano.
Haya yamefichuliwa Jumatatu na Waziri wa biashara Salim Mvurya, alipokutana na balozi wa Kenya nchini Qatar Mohammed Mutair al Enazi afisini mwake.
Mvurya na Mutair walijadilaina kwa kina kuhusu ushirikiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili na njia za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara.