Kenya yaipakata Mexico Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imeilabua Mexico mabao 2-1 katika mchuano wa mwisho wa kundi C na kusajili ushindi wa kwanza katika makala ya nane ya Kombe la Dunia kwa mabanati chini ya umri wa miaka 17.

Mchuano huo umesakatwa mapema Alhamisi katika uchanjaa wa Felix Sanchez mjini Santo Domingo, Jamhuri ya Dominica .

Valerie Nekesa na Lornah Faith walitikisa nyavu kunako dakika za 15 na 36 mtawalia,kabla ya Alexa Soto kukomboa moja kwa Mexico dakika za lala salama.

Lorna Faith pia alituzwa mwanandinga bora wa mechi hiyo.

Korea Kaskazini imeongoza kundi hilo lwa pointi 9, ikifuatwa na Uingereza kwa alama 6, huku Kenya ikiwa ya tatu kwa alama 3, kisha Mexico wakaburura mkia pasi na alama.

Kenya chini ya kocha Mildred Cheche ilikuwa inashiriki fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Zambia pia waliyaaga mashindano baada ya kupoteza mechi zote tatu, huku Nigeria wakiwa waakilishi pekee wa Afrika kujikatia tiketi kwa robo fainali.

Website |  + posts
Share This Article