Wenyeji Kenya waligutushwa baada ya Uganda kutoka nyuma na kuwacharaza mabao 2-1,kwenye fainali ya kombe la CECAFA kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18, iliyosakatwa Ijumaa katika uwanja wa Jomo Kenyatta Mamboleo kaunti ya Kisumu.
Cyprus Owuor alifungua ukurasa wa Kenya kwa bao la kwnza kunako kipindi cha pili kabla ya Batiibwe Okelo kukomboa bao hilo dakika 12,kabla ya kipenga cha mwisho na kulazimu mchuano kuamuliwa kupitia penati.
Ililazimu dakika 30 kuongezwa ili kutengamisha majimbi hao lakink punde tu baada ya sekunde 50 za nyongeza, Hakim Mutebi alicheka na nyavu kwa goli la ushindi.
Uganda walituzwa shilingi milioni 2 nukta 4 kwa ubingwa huo huku Kenya waliokuwa hawajashinfwa mechi wakiridhia medali ya fedha.
Tanzania ilimaliza ya tatu baada ya kuwazidia maarufa Rwanda mabao 3-1 katika mchuano wa afasi ya tatu na nne.