Kenya wang’atwa nyumbani na Nge wa Gambia

Ryan Ogam alipachika bao pekee la kufutia machozi kwa Kenya dakika 9 kabla ya kipenga cha mwisho.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ndoto ya Harambee Stars, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza imezimwa Ijumaa Alasiri baada ya kuambulia kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Gambia, katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

The Scorpion walianza vyema mechi hiyo huku wakichukua uongozi kunako dakika 12 kupitia kwa Sheriff Sinyan kabla ya Yankuba Minteh kuongeza la pili dakika ya 26 naye Musa Barrow akahitimisha ushindi kunako dakika ya 38.

Ryan Ogam alipachika bao pekee la kufutia machozi kwa Kenya dakika 9 kabla ya kipenga cha mwisho.

Kenya watarejea uwanjani Jumanne ijayo dhidi ya Ushelisheli.

Kichapo hicho kinazima ndoto ya Harambee Stars kufuzu kwa Kombe la Dunia moja kwa moja au kupitia mechi za mchujo.

Website |  + posts
Share This Article