Kenya tayari kuandaa maadhimisho ya siku ya Kiswahili Duniani

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya iko tayari kuandaa  maadhimisho ya  siku ya Kiswahili Duniani tarehe 7 mwezi ujao kwa mara ya kwanza.

Waziri wa jinsia,utamaduni,sanaa na turathi Aisha Jumwa siku ya Jumatano alibuni kamati ya  wanachama 17, kupanga hafla hiyo itakayoandaliwa Julai 5 na 6, huku  kilele chake ikiwa Julai 7 katika kaunti ya Mombasa.

Itakuwa mara ya tatu ya kuadhimishwa kwa siku  ya Kiswahili Duniani,tangu ianzishwe mwaka 2022.

Rais William Ruto anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima wakati wa sherehe hizo.

Zanzibar iliandaa sherehe za kwanza mwaka 2022, kabla ya Uganda kuwa mwenyeji mwaka 2023 jijini Kampala .

Shirika la Umoja wa mataifa linalohusiana na Sayansi , Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwenye kikao chake cha mwaka 2022 jijini Paris, Ufaransa, liliidhinisha Julai 7 kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya Kiswahili.

Hii ni mojawapo ya mikakati ambayo inaendelea inayolenga kufanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya mataifa ya Jumuiya  ya Afrika Mashariki.

 

Website |  + posts
Share This Article