Timu ya mpira wa wavu ya Kenya Prisons ndio mabingwa wa mashindano ya mpira wa wavu ya Gavana Mwalimu Kahiga, baada ya kuilaza Kenya Pipeline seti tatu kwa mbili kwenye mechi ya kusisimua iliyochezwa katika uwanja wa Kamukunji kaunti ya Nyeri.
Kenya Prisons waliwapiga mabingwa wa ligi kuu ya mpira wa wavu KCB seti tatu kwa bila, seti za alama 25-20,25-13 na 25-22 kwenye nusu fainali, huku Kenya Pipeline ikiilemea DCI seti 3-2, seti za alama 26-28,27-25,22-25,25-14 na 15-10.
GSU iliilaza KPA kwenye semi fainali ya wanaume wakimenyana kwenye fainali na KDF ilioilaza Kenya Prisons kwenye mechi nyingine ya nusu fainali.
Washindi walizawadiwa shilingi 50,000 huku aliyemaliza wa pili na tatu akiondoka na kitita cha shilingi 30,000 na 20,000 mtawalia.