Kenya na Urusi zaambulia sare ya 2-2 mechi ya kirafiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imetoka sare ya mabao 2-2, na Urusi katika mchuano wa kirafiki uliopigwa Jumatatu jioni katika uwanja wa Olympic mjini Antalya Uturuki.

Urusi wakichukua uongozi kunako dakika ya nane kupitia kwa Alexander Sobolev, kabla ya Anthony Akumu, kusawazisha kwa vijana wa Ke ya katika dakika ya 16 naye Masud Juma, akapiga goli la dakika ya 36 na kuhakikisha Harambee Stars wanaongoza 2-1 kufikia mapumzikoni.

Licha ya Harambee Stars kudhihirisha mchezo wa hali ya juu,Urusi walifanya mabadiliko na kuimarisha mchezo na baadaye Ivan Oblyakov akakomboa goli kunako dakika ya 86.

Kenya ilitumia mchuano huo kujiandaa kwa mechi ya kwanza ya kundi F, kufuzu kwa fainali za kombe la dunia tarehe 13 mwezi ujao dhidi ya Gabon.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article